Saturday 16 July 2016

WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA WAJISALIMISHA

WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA 60,000 WAJISALIMISHA BAADA YA RAIS KUAGIZA WAUAWE POPOTE WALIPO


Takribani watumiaji wa dawa za kulevya 60,000 wamejisalimisha kwenye mamalaka husika baada ya Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino kuwaambia wananchi wawaue popote pale watakapowaona.


Rais huyo ambaye alishinda uchaguzi wa Mei mwaka huu, aliahidi kupammbana na dawa za kulevya ndani ya nchi hiyo. Alisema kuwa wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya wamekuwa wakiwaharibu watu wengine ambao hawatumii.


Jeshi la Polisi nchini humo limeeleza kuwa watu 110 wanaohusishwa na dawa za kulevya wameshauawa tangu Rais huyo alipoingia madarakani lakini vyombo vya habari vya ndani vimesema kuwa idadi ya waliouawa wanakaribia 200.


Rais Rodrigo ameonya huenda damu zaidi ikamwagika ikiwa ni njia ya kuhakikisha kuwa habari za dawa za kulevya zinakwisha. Ameahidi kuwalinda Polisi dhidi ya sheria pale watakapomuua polisi.





RIHANNA

RIHANNATENSE MOMENTS AFTER NICE MASSACRE

Rihanna was in the middle of dinner at a restaurant in Nice when she learned 84 people were slaughtered just 20 minutes away.
We got these pics of the singer, whose scheduled concert Friday night was cancelled out of respect and security concerns.
Rihanna was fixated on her phone, presumably trying to figure out what to do in the wake of the murders.

UTATA WA PICHA

PICHA YA RAIS JACOB ZUMA WA AFRIKA KUSINI AKIMBUSU MSICHANA YAZUA UTATA


Picha inayoaminika kuwa ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akumbusu msichana anayeelezwa kuwa na umri wa miaka 19, imezua gumzo nchini Afrika Kusini.
Msichana huyo aliweka picha hii katika mtandao  wa Facebook na kuandika “he is not just a blesser, we are deeply inlove and am greatful for all that he has done for me, much love. Xo xo.”

Raia wengine wa Afrika Kusini wanaeleza kuwa hawakushtushwa na picha hiyo kwani walidai Rais huyo ni mtu anayependa sana mambo hayo hivyo siyo jambo geni sana kwao.
Baada ya muda mfupi picha hiyo kuwekwa, akaunti ya msichana huyo haikuonekana tena na wengi wakiamini kuwa iliondolewa kwa agizo la Rais Zuma.
Rais Zuma alipotafutwa kuzungumza kuhusu hili alijibu kuwa “we will check the matter.”


JARIBIO LA MAPINDUZI YA KIJESHI SERIKALI YA UTURUKI

WATU 66 WAUAWA, MAMIA WASHIKILIWA KATIKA JARIBIO LA KUPINDUA SERIKALI UTURUKI


Takaribani watu 60 wameuawa nchini Uturuki huku wengine 336 wakishikiliwa na Jeshi la nchini hiyo kufuatia tukio la usiku wa kuamkia leo Julai 16 ambapo kulikkuwa na jaribio la kutaka kupindua serikali ya nchi hiyo.


Usiku wa kuamkia Julai 16 kwa saa za Afrika Mashariki, kikundi cha Wananjeshi wa Uturuki kilitangaza kupitia televisheni kuwa wamepindua serikali ya nchi hiyo na kuwa wao ndio wapo madarakani.
Muda mfupi baadae Waziri Mkuu wa nchi hiyo alizungumza na kusema kuwa, serikali hiyo iliyokuachaguliwa na watu itaendelea kuwa madarakani hadi pale wananchi walioichagua kuamua kuwa sasa iondoke na si vinginevyo.

Wakati wa tukio hilo, mitandao ya kijamii ilifungwa, viwanja vya ndege vilfungwa na nchi kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Katika hatua nyingine, Mku wa Jeshi la Uturuki alikuwa akishikiliwa na kikundi kilichojaribi kupindua serikali.
Rais wa Uturuki,  Recep Tayyip Erdoğan ametangaza na kusema kuwa jaribio la kupindua serikali limeshindwa na sasa mambo ni shwari.



RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI

TAARIFA: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI, AUGUSTINO LYATONGA MREMA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
  1. Augustino Lyatonga Mrema.
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
  • Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.

  1. William R. Mahalu
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

  1. Mohamed Janabi
  • Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  1. Angelo Mtitu Mapunda
  • Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  1. Sengiro Mulebya
  • Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  1. Oliva Joseph Mhaiki
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  1. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
  • Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  1. Charles Rukiko Majinge
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

  1. Julius David Mwaiselage
  • Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.


Kupandishwa Vyeo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1. Essaka Ndege Mugasa
  2. Adamson Afwilile Mponi
  3. Charles Ndalahwa Julius Kenyela
  4. Richard Malika Revocatus
  5. Geofrey Yesaya Kamwela
  6. Lucas John Mkondya
  7. John Mondoka Gudaba
  8. Matanga Renatus Mbushi
  9. Frasser Rweyemamu Kashai
  10. Ferdinand Elias Mtui
  11. Germanus Yotham Muhume
  12. Fulgence Clemence Ngonyani
  13. Modestus Gasper Lyimo
  14. Mboje John Shadrack Kanga
  15. Gabriel G.A. Njau
  16. Ahmed Zahor Msangi
  17. Anthony Jonas Rutashubulugukwa
  18. Dhahir Athuman Kidavashari
  19. Ndalo Nicholus Shihango
  20. Shaaban Mrai Hiki
  21. Simon Thomas Chillery
  22. Leonard Lwabuzara Paul
  23. Ahmada Abdalla Khamis
  24. Aziz Juma Mohamed
  25. Juma Yussuf Ally

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1. Fortunatus Media Musilimu
  2. Goyayi Mabula Goyayi
  3. Gabriel Joseph Mukungu
  4. Ally Omary Ally
  5. Edward Selestine Bukombe
  6. Sifael Anase Mkonyi
  7. Naftari J. Mantamba
  8. Onesmo Manase Lyanga
  9. Paul Tresphory Kasabago
  10. Dadid Mshahara Hiza
  11. Robert Mayala
  12. Lazaro Benedict Mambosasa
  13. Camilius M. Wambura
  14. Mihayo Kagoro Msikhela
  15. Ramadhani Athumani Mungi
  16. Henry Mwaibambe Sikoki
  17. Renata Michael Mzinga
  18. Suzan Salome Kaganda
  19. Neema M. Mwanga
  20. Mponjoli Lotson
  21. Benedict Michael Wakulyamba
  22. Wilbroad William Mtafungwa
  23. Gemini Sebastian Mushi
  24. Peter Charles Kakamba
  25. Ramadhan Ng’anzi Hassan
  26. Christopher Cyprian Fuime
  27. Charles Philip Ulaya
  28. Gilles Bilabaye Muroto
  29. Mwamini Marco Lwantale
  30. Allute Yusufu Makita
  31. Kheriyangu Mgeni Khamis
  32. Nassor Ali Mohammed
  33. Salehe Mohamed Salehe
  34. Mohamed Sheikhan Mohamed
Maafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Julai, 2016

UKIUKWAJI WA MAADILI


BASATA YAUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO


Baraza ka Sanaa nchini (BASATA) limeufungia wimbo wa mwanamuziki Nay wa Mitego unaokwenda kwa jina la Pale kati Patamu kwa maelezo kuwa wimbo huo kwa kiasi kikubwa umekiuka maadili ya sanaa na jamii kwa ujumla.
Nay wa Mitego imeelezwa kuwa amekuwa akitoa nyimbo na kufanya matamasha ya muziki ambayo si kwamba ni kinyume na maadili ya Tanzania lakini pia amekuwa akiwadhailisha wanawake kwa picha anazopiga na maneno anayoyaumia katika nyimbo zake.
Nay wa Mitego hivi karibuni emetoa wimbo wake wa Pale Katipatamu ambao picha za wimbo huu zimesambaa mitandaoni zikionyesha wasichana waliopiga picha wakiwa utupu kitu ambacho si sawa.
BASATA limewakumbusha wasanii woe nchini kufanya kazi kufuatana na taratibu zilizopo lakini pia kuangalia maadali ya nchi ili kuhakikisha kuwa mikwaruzano isiyokuwa yalazima inaepukika na kunakua na ushirikiano wa kuinua tasnia nzima ya sanaa nchini.


















Wednesday 6 July 2016

WA-AFRIKA WANAOREJEA KUTOKA UGHAIBUNI

sababu ya BAADHI YA WA-AFRIKA WANAREJEA NYUMBANI KUTOKA UGHAIBUNI.


atu wengi sana kutoka barani Afrika wamekuwa wakizunguka katika nchi nyingi na mabara tofauti lakini mara zote, Ulaya na Amerika ya Kaskazini ni maeneo mawili ambapo wa-Afrika wengi wamevutiwa kwenda kuishi ambapo takribani wahamiaji milioni 8.8 wanaishi katika maeneo hayo mawili.
Kuanzia mwaka jana, kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kukata tiketi za moja kwa moja za kurudi makwao na kuiaga Marekani, Canada na bara Ulaya.
Waafrika wengi waliopo nchi za magharibi wanasoma au wanafanyakazi huku wakifurahia maisha mazuri ya huko,. Lakini bado wamekuwa ni nguzo muhimu ya uchumi wa Afrika kwani kwa mwaka 2012 inaelezwa kuwa kiasi cha fedha dola bilioni 64.3 zilitumwa na wa-Afrika waishio nje.
Kupata visa ya kusafiria si kazi ndogo, ndio maana inashangaza sana kuona raia kutoka Afrika waliopo nje ya nchi wakikubali kwa maamuzi yao wenyewe kurejea makwao. Lakini ukweli ni kuwa kuna sababu kwanini wanakubali kurudi makwao.
Baadhi ya wanaorejea Afrika wameeleza kuwa wanarudi kutokana na fursa zilizopo katika mataifa mengi ya Afrika yanayokua kiuchumi na kuwa wanaamini uzoefu na ujuzi walioupata kutoka ughaibuni utawasaidia kuchangia maendeleo ya nchi zao.
Wengine wamenukuliwa wakisema kuwa wanarejea Afrika kwa sababu ya uzalendo. Kama kundi lililopita walivyoeleza, hawa nao wanaamini wana wajibu wa kuitumikia jamii yao baaada ya kupata ujuzi kutoka katika nchi za magharibi. Baadhi ya hawa ni madaktari, maprofesa.
Kundi jingine lilieleza kuwa wao wanarudi nyumbani (Afrika) kwa sababu ya wale waliowaacha nyuma wakati wakienda ughaibuni. Walisema kuwa waliwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki zao na kuona kuwa familia yao kubwa iko Afrika hivyo waliamka siku na kuona bora wabebe vyao na kurudi kuungana na familia zao.
Inaelezwa kuwa wengi wanaporejea kutoka ughaibuni wanapata changamoto nyingi sana ikiwa na pamoja na watu kuamini kuwa ukitoka ughaiuni basi utakuwa na fedha nyingi sana za kumpa kila mmoja. Lakini wengine wamekumbana na changamoto katika utendaji wa serikali. Hawa wamesema kuwa serikali za magharibi zipo makini na kuwa inawawia vigumu wao kuishi Afrika ambapo serikali hazipo makini na wakati mwingine huamua kurudi ughaibuni.

BEI MPYA ZA MAFUTA

 BEI MPYA ZA MAFUTA KUTOKA EWURA
  
EWURA ilitangaza  bei mpya za mafuta Jana tarehe Julai 5 ambapo  kuanzia kutumika Jumatano Julai 6 ikiwa ni mabadiliko ya gharama katika soko la dunia.
Zifuatazo ni bei halisi za Mafuta kutoka EWURA
    • > Petrol inauzwa kwa shilingi 1,888 badala ya bei ya awali ambayo ilikuwa ni shilingi 1,865,
  • > Diesel inauzwa kwa shilingi 1,720 badala ya bei ya awali ambayo ilikuwa ni shilingi 1,633 na
  • > Mafuta ya taa yanauzwa shilingi 1,687 badala ya bei ya awali ambayo ni shilingi 1,607.





OSCAR PISTORIUS MAHAKAMANI

LIVE: TAZAMA HUKUMU YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS MAHAKAMANI

HUDDAH MONROE AFUNGUKA

VIDEO: HUDDAH MONROE AFUNGUKA KUHUSU BOYFRIEND WAKE




Baada ya kuonekana muda mwingi akila bata peke yake na mara kadhaa na marafiki zake wakike, mlimbwende Hudda kutoka Kenya afunguka kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi.

TAZAMA VIDEO 

ABIRIA ASAHAU MA MILLIONI YA HELA KWENYE TAXI

ABIRIA ASAHAU SHILINGI MILIONI 375 KWENYE TAXI, SOMA ALICHOKIFANYA DEREVA TAXI.



Je! Mtu akisahau kitita cha fedha nyumbani au kwenye gari lako utafanyaje? Soma kisa cha dereva taxi huyu.
Dereva taxi mmoja nchini Marekani, Raymond MacCausland maarufu “Buzzy,”siku ya Jumamosi alikumbana na bahati kubwa baada ya kukuta fedha nyingi kwenye siti ya nyuma ya gari lake baada ya abiria aliyekuwepo kuzisahau.Dereva huyo alikuta abiria wake aliyempeleka eneo la Boston USA, alisahau $187,000 (TZS milioni 375). Kilichowashangaza wengi ni uamuzi aliouchukua dereva huyo mara alipoona fedha hizo.

Buzzy aliamua kuzipeleka fedha hizo katika kituo cha Polisi Boston na Polisi walisema kuwa fedha hizo ni mali ya mwanaume mmoja ambaye amezipata baada ya kuuza mali za urithi.
Dereva huyo alipohojiwa kuhusu uamuzi wake huo alisema kuwa hivyo ndivyo alivyolelewa kuwa mwaminifu na ametenda kama alivyopaswa kutenda. Aidha, amesema kuwa alizikuta fedha hizo alipokuwa akitafuta baadhi ya vitambulisho kwenye gari lake.Mwenye fedha hizo alimpatia dereva huyo kiasi cha USD 100 kama shukrani kwa uaminifu wake.



WASICHANA CONGO WATUMIA DAWA ZA KUREJESHA BIKIRA

WASICHANA CONGO WATUMIA DAWA KUREJESHA BIKIRA ZAO, JE! DAWA INAFANYA KAZI?


Baadhi ya wanawake nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wanadaiwa kutumia dawa ili kurejesha tena ubikira wao kwa lengo la kujiongezea thamani wakati wanapofunga ndoa.
Inaaminika kuwa hicho ni moja ya vigezo muhimu kuonyesha kuwa msichana alikua na kulelewa katika maadili mazuri nyumbani kwao kwa mjibu wa mila na desturi zao.
Je dawa hizi zipo?
Je dawa hizo zinaweza kurejesha heshima hiyo hata kama msichana alikuwa kwenye mahusiano tayari?

LIONEL MESSI JELA INAMUHUSU

LIONEL MESSI AHUKUMIWA KIFUNGO JELA
Mchezaji mpira wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukimwa kwenda jela miezi 21 kwa kosa la kukwepa kodi na Hukumu ya aina hiyo hiyo imetolewa na kwa Baba yake, Jorge Horacio Messi.
Aidha kwa Sheria ya Hispania, Hukumu yoyote chini ya miaka 2 inaweza kuahirishwa hivyo basi Mchezaji huyo anawekana asitumikie kufungo hicho. Messi alipofikishwa Mahakamani alijitetea kwa kusema kwamba. ‘Nilikua sina habari ya jambo lolote wakati nacheza mpira, na nilimuamini Baba yangu na Mwanasheria wangu’Alikua anatuhumiwa kwa kuanzisha Makampuni feki huko Belize na Urugwai ili akwepe kulipa kodi ya €4.16m (£3.2m) kati ya mwaka 2007 na 2008.

SABABU YA MKUU WA WILAYA TEULE WA MBOZI KUKATAA NAFASI HIYO

HII NDIYO SABABU YA MKUU WA WILAYA MTEULE WA MBOZI KUIKATAA NAFASI HIYO?


Mkuu wa Wilaya (DC) Mteule wa Mbozi, Ally Masoud Maswanya ajiondoa katika nafasi hiyo ya ukuu wa wilaya na badala yake, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa, John Ernest Palingo anakwenda kuwa DC Mbozi, na Kongwa itasubiri uteuzi mpya.


Kutoka kwenye mitandao ya kijamii, inadaiwa kuwa Ally Masoud Maswanya ambaye ni Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa mshahara wake anapokea baada ya makato yote ni milioni 20 hapo ikiwa bado hajapewa nyongeza (bonus) na marupu rupu mengine. Aidha inadaiwa kuwa kila baada ya miezi mitatu anapewa bonus ya kati ya shilingi milioni 10-15.
Watu wamedai kuwa hii ndio huenda ikawa na sababu ya Masoud kuubwaga ukuu wa wilaya. Inaelezwa kuwa maslahi anayayoyapata akiwa Tigo hawezi kuyapata akiwa serikali na pia ukichangia serikali ya awamu yatano ni Hapa Kazi Tu, basi kibarua chako kinakuwa hatarini muda wote

D'BANJ AFUNGA PINGU ZA MAISHA

D'BANJ MWANAMZIKI WA NIGERIA AFUNGA PINGU ZA MAISHA
Mwanamuziki kutoka Nigeria maarufu kama D’banj ameshangaza wengi baada ya taarifa za yeye kufunga pingu za maisha weekend iliyopita kusambaa.
Watu walishangaa kuona picha aliyopost kwenye mitandao ya jamii mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa amevaa pete na badae kukanushwa na kusema ile ilikua ni pete ya fasheni tu.
 Inasemekana kwamba D’banj amefunga ndoa na mtangazaji wa MTV katika kipindi cha Lip Sync Battle Didi Kilgrow, Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya kuzaliwa Baba wa mwanamuziki huyo.

Mpaka leo ‘The Kokomaster’ ambalo ni jina lingine la D’banj hajatoa statement yoyote kuhusu tetesi hizo, lakini Pongezi za kufunga ndoa bado zinaendelea kutoka kwa mashabiki wake.






WEMA SEPETU AFUNGUKA

BAADA YA DIAMOND KUMPOST WEMA SEPETU INSTAGRAM, WEMA AFUNGUKA JUU YA HILO KIUNAGA UBAGA.


Jana Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz alipost picha ya Wema Sepetu katika ukurasa wake wa Instagram akiwataka watu wajitokeze kumsupport katika tamasha. Pamoja na Wema Sepetu, Diamond alimpost pia Idris Sultan na Christian Bella.
Bonyeza hapa  kwa taarifa kamili kuhusu habari hiyo.

Wema Sepetu alipohojiwa kuhusu kitendo hicho alisema kuwa amefurahi sana na kuona kama kuna mzigo alioutua kwani watu walikuwa wakitumia tofauti zao za kutengenezwa kama faida kwao ili kupata wafuasi (Followers).
Aidha, ameeleza kuwa yeye ni shabiki wa Diamond Platnumz na amekuwa akisikiliza nyimbo zake hata baada ya wao kuachana. Amesema kuachana kwao hakumfanyi asiwe shabiki wake.
Alieleza kuwa kwa muda sasa amekuwa akijizuia kuimba nyimbo za Diamond akiwa kwenye public lakini ameona kuwa anajikomoa yeye mwenyewe kwani akirudi kwenye gari lake huwa anaimba. Kwake amesema kuwa kitendo hicho kinaondoa uongo uliokuwa unasemwa kwamba wawili hao wana bifu zito.

DIAMOND AM-POST WEMA SEPETU

HATIMAYE DIAMOND PLATNUMZ AMEM POST WEMA SEPETU


CAPTION: diamondplatnumzMake sure ya' all go Support Christian Bella X Wema Sepetu X Idris Sultan na wengine wakali kibao katika Usiku wa #BlackTie pale King Solomon Hall tareh 9 / 07 /2016!!! It's all about Black and Everything!